Jumanne , 21st Jun , 2022

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, mtoto wa tajiri namba 1 duniani anayefahamika kwa jina la Xavier Alexander Musk amepeleka ombi mahakamani la kubadilisha majina yake na kukata mahusiano na Elon Musk kama mzazi wake.

Elon Musk

Xavier ambaye ana umri wa miaka 18 alipeleka ombi hilo katika mahakama moja huko Los Angeles katika mji wa California, Marekani.

Katika ombi hilo pia anataka kutambulika rasmi kama mwanamke baada ya kubadilisha jinsia, na kuitwa Vivian Jenna Wilson ambapo atatumia jina la mama yake anayeitwa Justine Wilson.