Alhamisi , 7th Mar , 2024

Raj Kumar raia kutokea nchini India amekamata vichwa vya habari ulimwenguni mwote baada ya madaktari kufanikiwa kupandikiza mikono.

 

Raj kumar ambaye ni mwana sanaa ya uchoraji kutokea nchini India, alipata ajali ya treni mwezi wa 10, 2020. Ajali ambayo ilipelekea kupoteza mikono yake yote miwili.

Jopo la madaktari 11 kutokea hospitali ya Sir Ganga Ram nchini India, walitumia takribani saa 12 kufanikisha upandikizaji wa mikono kwa bwana Raj kumar...

..mikono ambayo ilikuwa sehemu ya sadaka ya Mwanamama kutokea nchini humo ambaye alipendekeza viungo vyake vitumike kwa wahitaji atakapo tangulia mbele ya haki.

Chanzo: The Tribune