Jumapili , 14th Jan , 2024

Mwanaume mmoja kutokea nchini Italia amejikuta akitembea umbali wa kutoka Dar es salaam mpaka Moshi kwa mguu baada ya kukosana na mkewe,

Mwanaume huyo ambaye jina lake halikuwekwa wazi alikutwa kwenye mji wa Fano akiwa ametokea kwenye mji wa Como umbali ambao unakadiriwa kuwa ni Miles 280, ambayo ni sawa na kilomita 450

Kwenye majira ya saa 8 usiku alikamatwa na polisi baada ya mkewe kutoa taarifa za kupotea kwake, na kwenye uchunguzi wa awali ikabainika ya kuwa alitembea umbali wa kilomita 64 kwa siku kufika kwenye mji wa Fano.

Image credit: Storyblocks Video

Chanzo: People