Jumatano , 25th Aug , 2021

Barabara kuu ya ghorofa tatu ya Tianlong iliyojengwa kando ya mlima wa Tianlong wenye urefu wa mita 1,370 huko Taiyuan, kaskazini magharibi mwa Mkoa wa Shanxi nchini China inajulikana kutokana na kuwa kivutio cha watalii.

Picha ya daraja la ghorofa tatu

Wakazi wengi wa Taifa hilo wamekuwa wakisafiri kwenda hadi kwenye eneo hilo la mlima ili kufanya utalii na kushea picha mbalimbali za matukio kwenye mitandao ya kijamii. 

Barabara hiyo yenye mita 350 na urefu wa kilomita 30 ilijengwa na wafanyakazi 3000 ili kurahisisha watalii kuingia katika eneo hilo huku inaelezwa kuwa walitumia miezi mitano tu kulikamilisha.