Jumanne , 10th Aug , 2021

Mchekeshaji Idris Sultan ameingia kwenye orodha ya ma-star wa dunia ambao wametengeneza pesa nyingi zaidi kupitia mtandao wa instagram kwa mwaka 2021 (Instagram Rich List) hii ni kwa mujibu wa tovuti ya Hopper HQ.

Picha ya Mchekeshaji Idris Sultan na Mwanasoka Cristiano Ronaldo

Idris ndiye Mtanzania pekee kwenye list hiyo akiwa anashika nafasi ya 108 duniani na ya 11 kwa Afrika huku akitajwa kutoza kiasi zaidi ya dola elfu 42 ambazo ni sawa na Tsh. Milioni 99.2 kwa post ya tangazo la biashara. 

Na mwanasoka Cristiano Ronaldo anaongoza kwa dunia akiwa anatoza zaidi ya dola Milioni 1.6 ambazo ni zaidi ya Tsh. Bilioni 3.7 huku kwa Afrika Mohamed Salah anaongoza kwa kutoza zaidi ya dola laki 231 ambazo ni sawa na Tsh. Milioni 533.7 kwa post.

Kwenye upande wa muziki, mwimbaji wa Nigeria, Davido yupo nafasi ya 53 na ya 2 kwa Afrika akiwa anatoza kiasi zaidi ya dola laki 128 sawa na Tsh. Milioni 296.4 kwa post ya Tangazo la biashara.