Jumanne , 16th Jan , 2024

Siku ya jana historia mpya iliandikwa asubuhi ilipambwa kwa jina la ''Asubuhi ya ahadi timilifu'' ilikuwa na mengi ndani yake, lakini namna rahisi ya kuieleza ni kama ndugu wamekutana kwa pamoja na wakazungumza yale yahusuyo ukuaji wao na wenzao kwa maslai mapana ya nchi.

 

Ndivyo ilivyokuwa Jana kwa kukutana na wana-familia ya #SUPABREAKFAST tumezungumza mengi kama familia, tukajadili mengi kwa niaba yako mwanafamilia ambaye ulikuwa na majukumu kidogo kwa leo lakini ulipata wasaa wa kuungana nasi kupitia #EastAfricaTv na #EastAfricaRadio

Hakuna neno kubwa zaidi ya Ahsante kwa muungwana, tuungane kwa pamoja kuelekea safari ya utekelezaji wa ahadi zitakazojazwa utimilifu.