Alhamisi , 12th Aug , 2021

Msanii wa Filamu za Bongo na Mjasiriamali, Muna Love amefanya upasuaji 'surgery' sehemu ya shavuni na kuweka dimpozi.

Picha ya Muna Love

Kupitia Instagram ameeleza kuwa alikuwa akipenda sana dimpozi ambapo hakubaatika kuwa nazo hivyo imembidi afanye upasuaji kuuridhisha moyo wake  na kuupa muonekano mpya sura yake.

Pia amesema hii ilikuwa ni surgery ya pili kati ya nne alizozifanya tayari ambazo ame ahidi kuziweka wazi muda wowote.