Alhamisi , 1st Feb , 2024

Viongozi na wamiliki wa mitandao ya kijamii ikiwemo META, TikTok na X waliitwa mbele ya Bunge la Marekani kwa ajili ya kuulizwa kuhusiana na usalama wa watoto wanapotumia mitandao ya kijamii,

Lakini ulifika wasaa ambao Seneta kutoka chama cha Republican Mh: Tom Cotton kuuliza swali kwa moja ya wamiliki hao na ikaangukia kwa Mmilikiwa wa mtandao wa TikTok ambaye ndiye mmiliki wa kampuni ya ByteDance Bw. Shou Zi Chew, ambaye kiasili alijinasibu kwamba yeye ni M-singapore ili hali kwa mtazamo na taswira iliyopo duniani inadhaniwa kuwa yeye ni M-china kwa utaifa.

Mambo yalikuwa hivi;
Mh: Tom Cotton: Umewahi kuwa mwanachana wa chama cha jumuiya ya ki-china (Chinese Communist Party)?

Bw. Shou Zi Chew: Hapana, Mimi ni raia wa Singapore.

Mh: Tom Cotton: Umewahi kujihusisha au kushirikiana na chama cha jumuiya ya ki-china (Chinese Communist Party)?

Bw. Shou Zi Chew: Hapana senator narudia tena mimi ni raia wa singapore
Mh: Tom Cotton: Wewe ni raia wa Taifa gani?

Bw. Shou Zi Chew: Singapore

Mh: Tom Cotton: Wewe ni raia wa taifa lingine?

Bw. Shou Zi Chew: Hapana

Mh: Tom Cotton: Umewahi kuomba uraia wa nchini China?

Bw. Shou Zi Chew: Senator, Nalitumikia taifa langu la Singapore, Hapana sijawahi.

Ni majibizano yaliyochukua dakika, huku senator Tom akiendelea kumuuliza maswali ya kumchokonoa Bw. Shou Zi Chew. Lakini Shou alishikilia msimamo wake wa kueleza kuwa yeye ni raia ya nchini Singapore na kusisitiza kwa kusema amelitumikia pia jeshi la singapore kwa miaka kadhaa kama ilivyo sheria ya nchini huko.

Unahisi Senator Tom alikuwa anahitaji kufahamu kitu gani kutoka kwa Bw. Shou Zi Chew au ni zile propaganda za kuwa mtandao huo unamilikiwa na china ndiyo zimemkaa kichwani?