Jumatano , 31st Jan , 2024

(Kumradhi) Kwa walioifia dini watakuwa si wageni kuhusu mwandishi wa ‘’Mathayo 11’’ yanayozungumzia kuhusu watu wasiyo uwezo wa kuona kupata kuona tena.

Hili ni tofauti kwa utendaji lakini linafanana kwa utekelezaji, na utofauti wake unatengenezwa na teknojia.

Elon Musk, kupitia kampuni yake ya Neuralink, anafanyia kazi teknolojia ya upandikizaji wa ubongo ambapo anasema kuwa teknolojia hiyo inaweza kurejesha uwezo wa mtu kuona hata kama alizaliwa pasi na uwezo wa kuona (kipofu)

Teknolojia hiyo inahusisha aina mpya ya upandikizaji wa ubongo ambayo hutumia waya nyembemba zilizo na umeme ndani yake yenye uwezo wa kupitisha taarifa za uwoni moja kwa moja kwenye ubongo kupitia njia za macho zilizoharibiwa.

Picha: businessinsider.com