Alhamisi , 22nd Feb , 2024

Siyo mara ya kwanza kwa mchele kuzungunza kwenye supatech na kama ulihisi ni utaratibu ambao upo Tanzania pekee basi utakuwa unakosea sana, kwani ni utaratibu wa Duniani kote mpaka inafika wakati kampuni za uzalishaji simu za mkononi zinatokakatazo

 

Kampuni ya Apple inc imetoa katazo kwa watumiaji wa simu za iPhone dhidi ya kutumia mchele kukausha iPhone ambazo zimeingia maji,

Kwani kufanya hivyo kunatajwa kuharibu simu kupitia chembe chembe zinazopatikana ndani ya mchele, badala yake kampuni hiyo imeshauri watumiaji wa simu hizo kugonga gonga kifaa hicho kwa upole kuruhusu unyevu kuondoka kwenye simu hizo huku ukiacha ikauke kwa nusu saa mpaka siku nzima ikiwa ni lazima.

Ila mimi nimepanga nikufahamishe mbinu moja wapo unayoweza kuitumia pale ambapo simu yako itakuwa imeingia maji na spika yako haitoi sauti

Simu yako imeingia maji?, spika yako inatoa sauti ambayo huipendi? sawa pole kwa changamoto hiyo karibu hapa kwa suluhisho.

Usipeleke simu kwa fundi kwanza, wala usiweke kwenye mchele, kama umekutana na changamoto tajwa hapo juu au za namna hiyo, 

Unachoweza kufanya

Ingia kwenye ''search engine'' mfano Google, Safari, Chrome na nyinginezo alafu andika ''Fixmyspeaker'' Link hii hapa  fixmyspeakers.com 

Ukishaingia utagusa kwenye ki-mchoro cha maji mfano pichani sogeza kushoto, utasikia sauti ikitoka hiyo sauti ndio itakufahamisha kwamba spika ya simu yako bado iko njema na pia itakusaidia kutoa maji yaliyomo kwenye spika.

Nje na hapo kama bado changamoto ni ile ile ni vyema ukaomba msaada kwa watu wako wa karibu.