Jumatano , 29th Oct , 2014

Chama cha mpira wa mikono nchini kimesema mwaka huu hawana ratiba ya kushiriki michuano ya kumuenzi baba wa Taifa Mwalimu Nyerere inayofahamika kama Nyerere Cup kutokana na kuwa na ratiba nyingi za michuano ya kumaliza mwaka.

Timu za Mpira wa Mikono zikiwa Uwanjani

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Mikono Nchini TAHA, Nicholaus Mihayo amesema mara nyingi michuano mbalimbali hushirikisha timu za jeshi, hivyo kutokana na kuwa na kuwa na michuano mingi kwa wakati mmoja timu hizo zisingeweza kushiriki michuano hiyo.

Mihayo amesema, timu za jeshi hutegemea bajeti kutoka serikalini hivyo kwa mwaka huu timu hizo zimeshindwa kutokana na kuwa na mashindano mengi ambayo yote yanahitaji fedha kwa ajili ya ushiriki wa michuano hiyo.