Jumamosi , 26th Jul , 2014

Chama cha mpira wa mikono Tanzania TAHA bado kina lia na ukata kwa ajili ya safari na kufanya maandalizi ya timu ya taifa ya mpira wa mikono itakayoshiriki michuano ya ubingwa kwa nchi za Afrika Mashariki na kati nchini Uganda.

Baadhi ya wachezaji wakichuana katika mechi ya mashindano ya afrika mashariki msimu uliopita.

Msafara wa watu 36 viongozi na wachezaji wa timu ya taifa ya mpira wa mikono ya Tanzania kwa upande wa wanaume unataraji kuondoka nchini August 12 mwaka huu kuelekea Kampala Uganda ambako timu hiyo itashiriki michuano ya kombe la challenge kwa nchi za afrika mashariki na kati ambayo itaanza August 15 mwaka huu

Katibu mkuu wa chama cha mpira wa mikono Tanzania TAHA Nicolaus Mihayo amesema taratibu zote za safari ziko vizuri na timu hiyo imeshaanza maandalizi mazito kwa ajili ya michuano hiyo ambayo msimu huu wameahidi kuibuka na ubingwa

Aidha Mihayo ametoa wito kwa wadau wa michezo na watanzania wote wenye uwezo wajitokeze kuisaidia timu hiyo kwa hali na mali katika kufanikisha maandalizi na safari ya timu hiyo ili iweze kufanya vema katika michuano hiyo.