Jumanne , 27th Mei , 2014

Klabu ya African Lyon ya Dar es Salaam inayoshiriki ligi daraja la kwanza imesema hivi sasa imeanza maandalizi ya ligi daraja la kwanza msimu ujao.

kikosi cha klabu ya African Lyon

Klabu ya soka ya African Lyon iko katika mawindo ya kujipanga kwa ajili ya ligi daraja la kwanza FDL msimu ujao ambapo kwa kuanzia wamewatema wachezaji saba waliokuwa na kikosi cha timu hiyo msimu uliopita kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kushuka viwango vyao.

Mmiliki wa klabu hiyo yenye maskani yake Mbagala jijini Dar es salaam Rahim Kangezi Zemunda amesema hawajakatishwa tamaa kwa kuikosa nafasi ya kurejea ligi kuu bara dakika za mwisho kwakuwa mpango wao ulikuwa ni kufanya hivyo baada ya miaka mitatu ili timu ikipanda daraja ikatoe ushindani badala ya kupanda na kushuka.