Alhamisi , 23rd Sep , 2021

Mshindi mara tatu wa Grand Slam, Muingereza Andy Murray amefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya mashindano ya Tennisi ya Moselle Open inayoendelea nchini Ufaransa baada ya kumfunga Mpoland Vasek Pospisil kwa seti 6-3 & 6-3 usiku wa kumkia leo.

Andy Murray akijaribu kuukosa mpira kwenye mashindano ya Moselle Open nchin Ufaransa.

Baada ya Andy Murray kutinga hatua hiyo, sasa anasubiri kucheza na mshindi wa mchezo wa mtoano wa 16 bora utakaowakutanisha Mfaransa Lucas Pouille na Hurkacz Hubert wa Poland usiku wa leo nchini humo.

Murray ambaye alicheza fainali ya Moselle Open mwaka 2007 amesema anachukulia mashindano hayo kama daraja la kurudisha ubora wake uliopungua makali mara baada ya kufanyiwa upasuaji mara  mbili na kumfanya awe nje ya uwanja kwa muda mrefu na kuporomoka kwenye viwango vya  ubora nchini England na Duniani.