Jumatatu , 7th Oct , 2019

Fainali ya pili ya Sprite Bball Kings 2019 imepigwa jana katika Uwanja wa Ndani wa Taifa na kushuhudia mabingwa watetezi Mchenga Bball Kings wakiendeleza ushindi.

Asha Baraka akimuelekeza jambo mwanaye Baraka Mopele

Katika mchezo huo, ilishuhudiwa staa wa Tamaduni, Baraka Mopele akicheza mbele ya mama yake ambaye ni mmiliki wa bendi ya Twanga Pepeta, Asha Baraka aliyekuja kumpa sapoti.

Kabla ya mchezo kuanza Asha Baraka alionekana na mwanaye akimpa maneno machache ya kumpa moyo na baada ya mchezo, aliingia na mpira katikati ya uwanja na kufunga pointi kadhaa.

Tamaduni imepoteza mchezo wa pili mfululizo wa fainali dhidi ya Mchenga Bball Stars, ambapo mchezo wa pili uliisha kwa Mchenga kuibuka na ushindi wa vikapu 104 dhidi ya 89 vya Tamaduni.

Mchezo wa tatu wa fainali unatarajia kupigwa kesho Jumanne, Oktoba 8 katika Uwanja wa Don Bosco Oysterbay. Endapo Mchenga itashinda mchezo huo itajihakikishia kunyakua ubingwa wa Sprite Bball Kings 2019, lakini endapo itapoteza mchezo huo, ratiba itaendelea katika mchezo wa nne.