Jumatano , 6th Jul , 2022

Klabu ya Azam imeendelea kukisuka kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao baada ya hii leo kumtambulisha aliyekuwa beki wa kulia wa Ruvu Shooting, Nathaniel Chilambo.

Beki wa kulia wa Ruvu Shooting, Nathaniel Chilambo.

Huu unakuwa ni usajili wa tatu kwa timu hiyo kwa wachezaji wazawa baada ya hapo awali kupata saini ya Cleophace Mkandala (Dodoma Jiji) na Abdul Suleiman 'Sopu' aliyetoka Coastal Union.

Kwa upande wa wachezaji wa kigeni walionaswa na matajiri hao wa Jiji la Dar es Salaam ni Kipre Junior (Sol FC), Tape Edinho (ES Bafing) wote kutoka Ivory Coast na kiungo mshambuliaji, Isah Ndala aliyetokea klabu ya Plateau ya Nigeria.

Azam FC chini ya Kocha wake Mkuu, Abdihamid Moallin imekuwa ikipendelea zaidi kuwapa nafasi vijana wadogo na wenye uwezo mkubwa.