Ijumaa , 25th Nov , 2022

kikosi cha Yanga jumamosi ya Novemba 25 ,2022 kinashuka dimbani kuvaana na Mbeya City katika uwanja wa Benjamin Mkapa kwenye mchezo wa ligi kuu Soka Tanzania bara utaochezwa majira ya saa 12:15 jioni.

Kuelekea katika mchezo huo kocha msaidizi wa Yanga SC Cedric Kaze ameongea na waandishi wa habari namna ambavyo amejiandaa

“Tumejiandaa vizuri kwa sababu tunajua Mbeya City mechi zao za karibuni wamefanya vizuri. Mechi yao ya mwisho katika uwanja wa Benjamini Mkapa uliopita tulitoka sare na walitupa changamoto ambayo tumejiandaa kuikabili tena”

“Kila mchezo kwetu ni muhimu, hatuna mchezo ambao tunaudharau ili tusipoteze malengo yetu. Ukifanya mzaha kwenye maandalizi lazima utaumbuka. Tunaheshimu timu zote za ligi kuu. Tunafahamu kila timu inatamani kutufunga hivyo tumejipanga vyema kuzuia hilo kutokea”

kwa upande mwingine kocha Kaze amesema kuwa  wachezaji walikosekana mchezo uliopita, wamerejea huku Baadhi ni kama  Aziz Ki, Djigui Diarra, kutoka kwenye majukumu ya timu za taifa. Yannick Bangala nae amerejea baada ya adhabu yake kuisha lakini tutamkosa Feisal Salum kutokana na kadi tatu za njano