Jumatano , 3rd Dec , 2014

Michuano ya Taifa ya Mchezo wa Baseball inatarajiwa kufanyika Desemba sita mpaka saba mwaka huu Uwanja wa shule ya Azania jijini Dar es salaam.

Michuano ya Taifa ya Mchezo wa Baseball inatarajiwa kufanyika Desemba sita mpaka saba mwaka huu katika uwanja wa shule ya Azania jijini Dar es salaam.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa mchezo huo Ahmed Makata amesema michuano hiyo inatarajia kushirikisha timu tano ambazo zipo katika makundi A na B.

Makata amesema baada ya michuano hiyo, timu hizo zinatarajia kushiriki michuano ya Afrika inayotarajiwa kufanyika Desemba 15 mpaka 20 Nairobi nchini Kenya ambapo itashirikisha nchi tano za Afrika ambazo ni Nigeria,Uganda, Afrika Kusini, Tanzania na wenyeji Kenya.