Jumatano , 5th Nov , 2014

Makamu wa Rais wa shirikisho la Ngumi za Ridhaa nchini BFT Wililo Robert pamoja na Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo Makore Mashaga wanatarajiwa kuelekea nchini Korea ya Kusini Novemba 11 mwaka huu kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Chama cha Ngumi Duniani AIBA

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu mkuu wa BFT, Makore Mashaga amesema AIBA ilitoa mualiko kwa viongozi watatu lakini kutokana na maandalizi ya mashindano ya Taifa yanayotarajiwa kufanyika Desemba Mosi mpaka Tisa, Rais wa Shirikisho hilo Mwita Rwakatare hatohudhuria mkutano huo.

Mashaga amesema mkutano huo utasaidia kuwasilisha changamoto zilizopo katika mchezo wa Ngumi ambapo kumekuwa na matatizo hususani kwa upande wa makocha wa mchezo huo hapa nchini.