Jumatano , 13th Oct , 2021

Kocha mkuu wa Biashara United, Patrick Odhiambo amesema kuwa kukosekana kwa nahodha wake Abdulmajid Mangalo kuelekea kwenye mchezo wa Ijumaa dhidi ya Al Ahli Tripoli, ni pigo kubwa kutokana na ubora wa beki huyo.

Kocha klabu ya Biashara United Mara, Patrick Odhiambo.

Mchezo huo wa raundi ya pili utapigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa majira ya saa 10:00 jioni, ambapo Mangalo atakosa mchezo kutokana na kutojumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji wakaocheza mashindano hayo.

Odhiambo ameweka wazi, kuwa Mangalo ni mchezaji anayewaunganisha wachezaji wenzake pindi anapokuwa uwanjani hii ikiwa ni pamoja na kuwa na uwezo mkubwa wa kuusoma mchezo pamoja kupandisha mashambulizi kama beki wa kati hii ikiwa pamoja na kufanya vizuri katika nafasi yake ya ulinzi.

Biashara wataingia katika mchezo huu wakiwa na kumbuku ya kupoteza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting kwa bao 1-0, ambapo Kocha Odhiambo amesema kuwa wamejipanga kuelekea mtanange ujao kwakuwa huo ushapita.

“Tumeyafanyia kazi makosa yetu, nimewaanda vijana wangu kisaikolojia na tumesahau mchezo uliopita na sasa tunaelekeza nguvu kwenye mchezo wa ijumaa, Oktoba25.”

“Mchezo dhidi ya Al Ahli Tripoli ni mchezo tofauti kabisa, nawafahamu vizuri nilicheza nao pindi nafundisha Gor Mahia, wanavijana ambao wananguvu, kasi na wepesi, ila sisi kama Biashara tumejipanga vizuri kushinda mchezo huo.’’ Amesema Odhiambo.

Kwa upande wa Al Ahli hawajacheza mchezo wowote wa ligi kuu msimu huu kwasababu ya machafuko ya kisiasa ambapo msimu uliopita wanandindanga hao kutoka Tripoli walipoteza kwenye fainali ya ligi ya Libya dhidi ya Al-Ittihad katika mikwaju ya penati.

Msimu uliopita, timu 24 za ligi kuu ya Libya ziligawanywa katika vikundi viwili ambapo kila kundi ilikuwana timu 12. Kiongozi wa kila kundi alikabiliana na washindi wa kundi lingine na washindi wa mikutano hiyo baadaye watakutana kwenye fainali.

Al Ahli alimaliza wa pili nyuma ya Al-Ittihad na kwa hivyo alikuja dhidi ya washindi wa Kundi A, Al Ahly Benghazi.