Alhamisi , 16th Oct , 2014

Bodi ya Ligi nchini Tanzania inatarajia kufanya mkutano wake wa kwanza Novemba 15 mwaka huu huku ikishirikisha viongozi wa vilabu shiriki vya Ligi Kuu na Ligi Daraja la kwanza.

Silas Mwakibinga-Afisa Mtendaji Bodi ya Ligi

Akizungumza na East Africa Radio, Afisa mtendaji wa Bodi ya Ligi, Silas Mwakibinga amesema mkutano huo ni wa kwanza ambapo lengo lake hasa ni kuhusu muundo mpya wa Bodi hiyo,Taarifa ya wakaguzi pamoja na uchaguzi mdogo.

Mwakibinga amesema taarifa kwa ajili ya mkutano huo zimeshatumwa kwa washiriki ili kuweza kuwapa nafasi kujiandaa kuhudhuria mkutano huo.