Jumanne , 21st Oct , 2014

Bodi ya ligi Tanzania TPLB imesema Mdhamni mkuu wa ligi kuu ya soka Tanzania bara VPL anatoa zawadi ya mchezaji bora wa kila mwezi na bado hawajaamua kutoka tuzo kwa makocha na waamuzi lakini hawajazuia mashabiki kutoa zawadi makocha au waamuzi

Kiungo wa Mbeya City Anthony Matogoro akiwa amenyanyua tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa tisa.

Bodi ya ligi Tanzania TPLB imekanusha na kutoa ufafanuzi juu ya zawadi aliyopatiwa kocha wa timu ya mbeya city Juma Mwambusi sambamba na zawadi aliyopewa mchezaji bora wa mwezi wa ligi mwezi wa tisa kiungo wa mbeya city Antony Matogoro

Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Silas Mwakibinga amesema makubaliano yaliyopo sasa na mdhamini wa ligi kuu ni kutoa zawadi ya mchezaji bora wa kila mwezi na sivinginevyo

Wakati huo huo Bodi ya ligi Tanzania TPLB imerizika na kazi inayofanywa na waamuzi wa ligi kuu ya soka Tanzania bara na kuwapongeza kwa kusimamia vema sheria 17 za soka kitu ambacho kimepunguza malalamiko kutoka kwa timu zinazoshiriki ligi kuu msimu huu

Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Silas Mwakibinga amesema umakini na utendaji wa haki kwa waamuzi wanaochezesha michezo ya ligi inayoendelea hivi sasa imekua ni chachu ya mabadiliko katika soka na kupelekea hata baadhi ya timu kupata ushindi ugenini na hivyo kuondoa dhana ya timu ngeni kuopata ushindi ugenini.