Jumamosi , 2nd Jul , 2016

Wasiwasi mkubwa umekikumba kikosi cha timu ya taifa ya riadha ya Jamaica kufuatia kuumia ghafla kwa mmoja wa wachezaji wake tegemeo Usain Bolt ambaye ameumia wakati wa mazoezi yake ya maandalizi ya michuano ya Olimpiki itakayofanyika Agasti mwaka huu

Mmoja wa Madaktari akimhudumia mwanariadha wa Jamaica wa Usain Bolt.

Mwanariadha nyota wa Jamaica, Usain Bolt ameumia nyama za paja wakati akiendelea na mazoezi yake ya maandalizi ya michuano ya Olimpiki ya Rio Brazil inayotarajiwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi wa nane mwaka huu.

Bolt ambaye ni bingwa wa dunia wa michuano mingi ya mbio duniani , ameumia wakati wa maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ambayo kimsingi ndiye alikuwa tegemeo namba moja la nchi ya Jamaica kutwaa medali za dhahabu katika michuano hiyo.

Hofu kwa kikosi cha Jamaica imetanda na maswali ya kama Bolt atakuwa fiti kwa ajili ya michezo hiyo itakayofanyika nchini Brazil yamekuwa yakiwaumiza kichwa Wajamaica lakini pia timu yake kwa ujumla.

Hata hivyo uhenda afya ya mwanariadha huyo bora duniani kwa sasa ambaye anatajwa kama ndiye binadamu pekee mwenye kasi ya ajabu aliyewahi kutokea katika karne hii ikaimarika hasa kufuatia kuanza kwa haraka matibabu yakuhakikisha mwanariadha huyo anarejea katika hali yake ya kawaida.