Alhamisi , 6th Nov , 2014

Baada ya kuwepo kwa malalamiko mengi katika mapambano mbalimbali ya ngumi za kulipwa nchini kwa nyakati tofauti wito umetolewa kwa mabondia kujifua kwa nguvu na kuhakikisha wanapata ushindi wa knock out ili kupunguza malalamiko ya kuonewa na majaji

Bondia Thomas Mashali kushoto akiwa katika moja ya mapambano yake

Kauli hiyo imetolewa na bondia bingwa wa zamani wa mikanda ya kimataifa ya UBO na IBF Afrika uzito wa kati Mtanzania Thomas Mashali ambapo amesema amelazimika kujifua vilivyo ili kuhakikisha mapambano yake yote atakayopigana anashinda kwa pigo la Knock out

Akizungumza na muhtasari wa michezo hii leo Mashali amesema mfano mzuri ameutoa hivi karibuni alipomtangwa Mkenya Andrew Wandera kwa Knock out ya raundi ya pili pigo ambalo linakua halina utata hasa pale inapotokea pambano linamalizika kwa majaji kutoa alama ndiko kunakoibua malalamiko

Mashali amesema ni vigumu kwa bondia hasa waliona majina makubwa kupata ushindi mara baada ya pambano kumalizika kwakua wengi wa majaji hua wanapenda kuwapa alama za juu mabondia chipukizi ili kuwainua kimchezo na hivyo mara nyingi ulazimika kutoa maamuzi yasiyo ya haki ili kuwabeba mabondia ambao wanakua wanataka waibuke na ushindi katika mpambano husika

Aidha Mashali amesemac dawa pekee ya kukomesha hali hiyo ni kuhakikisha bondia husika unakua uko fiti kwa asilimia 100% na hatimaye kuibuka na ushindi wa knock out katika mpambano huo kitu ambacho kinakua hakina utata wala zengwe kwani mshindi anaamuliwa moja kwa moja tofauti na kumwacha mpinzani wako akimaliza raundi zote ndipo mshindi aamuliwe kutokana na alama za majaji kitu ambacho mara kwa mara kimekua kikizua manung'uniko toka kwa baadhi ya mabondia ambao mara nyingi uhisi wanaonewa na majaji.