Jumatatu , 27th Jun , 2016

Ni kama mkosi kwa timu ya taifa ya Argentina na mshambuliaji wake mahiri Lionel Messi hii ni baada ya kuendelea kusotea mataji makubwa kufuatia kupoteza kwa mara nyingine mchezo muhimu wa fainali ya kombe la CopAmerica dhidi ya Chile alfajili ya leo.

Wachezaji wa timu ya Chile wakishangilia wakiwa na kombe lao la ubingwa wa michuano maalumu ya Copa America.

Argentina imehitimisha miaka 23 bila kupata kombe lolote na Messi alikuwa na nafasi kubwa ya kushinda angalau mara moja hasa katika michuano ijayo ya kombe la dunia itakayofanyika mwaka 2018 nichini Urusi akiwa na miaka 31 lakini hilo halitafikiwa tena hii ni baada ya mshambuliaji huyo kuamua kustaafu kuichezea timu hiyo.

Argentina wamepoteza fainali tatu mfululizo ndani ya miaka mitatu hii wakianza na fainali a kombe la dinia mwaka 2014 wakicheza na Ujerumani, mwaka jana 2015 walifungwa katika fainali ya kombe la Copa America dhidi ya Chile, inauma sana Messi alisikika akiwambia wenzake wakati akiwaagaa rasmi na kuachana na soka la kimataifa kwa ngazi ya timu za taifa.

Chile, ambayo ilisubiri kwa takribani miaka 99 ili kushinda kombe la Copa America, walifanikiwa kutwaa taji hilo nyumbani kwao katika mji wa Santiago na sasa tena wamefanya hivyo nchini Marekani katika mji wa New Jersey, lakini safari hii ikiwa ni michuano maalumu ya maadhimisho ya miaka 100 ya michuano ya Copa America, ni rekodi ya aina yake kwa kizazi kipya cha dhahabu cha Chile na wamefanikiwa.

Mchezo huo wa fainali iliyotawaliwa na mchezo wa ufundi na nguvu nyingi na rafu za hapa na pale ulidumu kwa dakika Dakika 120 baada ya awali kushuhudia timu hizo kucheza dakika 90 bila kuona mlango wa mwingine na hali hiyo ilikuwa hata katika dakika 30 za nyongeza za muda wa ziada wa mchezo huo ambazo nazo zilishuhudia timu hizo zikienda suluhu ya bila kufungana.

Katika mchezo huo ambao kwa kiasi kikubwa ulitawaliwa na ubabe wa hapa na pale huku ikushuhudiwa timu zote mbili zikimaliza kipindi cha kwanza zikiwa na wachezaji 10 baada ya Marcelo Diaz wa Chile kulambwa kadi mbili za njano na kuwa nyekundu dakika ya 28 kabla ya Marcos Rojo wa Argentina baadaye naye kutolewa nje kunako dakika dakika ya 43 kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja.

Baada ya kumalizika kwa muda wa dakika 120 ndipo ilipofikia hatua ya upigaji wa penati ili kuamua bingwa mpya wa michuano hiyo maalumu ambayo imefanyika kwa mara ya kwanza tena ikifanyika nje ya bara la Amerika ya Kusini nchini Marekani ikishirikisha mataifa 16 kutoka mabara ya Amerika Kusini, Kaskazini na Kati na Caribbean.

Katika zoezi la upigaji wa penati, Chile ndiyo walioanza ambapo kiungo fundi mkabaji Arturo Vidal alianza kwa kukosa mkwaju wake wa penati na baadaye mshambuliaji hatari wa Argentina Lionel Messi na kiungo Lucas Biglia nao walikosa penati zao kwa upande wa Argentina.

Hii inakuwa fainali ya pili ndani ya miaka miwili kwa timu hizi mbili kukutana katika hatua ya fainali ambapo mara zote mbili Chile wamechukuwa kikombe hicho kwa mikwaju ya penalti.

Fainali hizi zilichezwa mwaka jana nchini Chile na kurudiwa mwaka huu zikiwa ni maadhimisho ya miaka 100 tongu kuanza kwa michuano hii mwaka 1916.