Ijumaa , 30th Mei , 2014

TCA yajipanga kuhakikisha U19 inanyakua tiketi ya fainali za dunia katika michuano ya kufuzu daraja la pili Afrika itakayofanyika Lusaka mwezi Agost mwaka huu.

Baadhi ya wachezaji wa cricket Tanzania wakishangilia katika moja ya michezo yao.

Chama cha Cricket Tanzania TCA kimesema timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 19 inaendelea vema na maandalizi ya michuano ya Afrika division 2 kusaka tiketi ya kucheza kombe la dunia ambapo TCA wanajipanga kuhakikisha timu hiyo inakwenda kufanya vema katika michuano hiyo itakayofanyika Lusaka Zambia mwezi Agost mwaka huu.

Mjumbe wa TCA ambaye pia ni kocha msaidizi wa timu hiyo Kharil Rhemtulah amesema kwakuzingatia hilo wameamua kuwapeleka Kenya wachezaji wawili kwaajili ya kuwaongezea ujuzi katika nafasi ambayo wanacheza kitu ambacho kitawasaidia katika uchezaji wao katika nafasi hiyo muhimu ya upande wa kuokoa mipira.