Ijumaa , 17th Jun , 2016

Baada ya kusimamishwa kwa muda kwa michuano ya ligi ya mpira wa wavu mkoa wa Dar es Salaam ili kupisha baadhi ya vilabu vilivyokuwa na majukumu ya kitaifa sasa michuano hiyo itaendelea kama ilivyotangazwa awali Julai o2 mwaka huu na sivinginevyo

Baadi ya wachezaji wakichuana katika moja ya michuano ya mpira wa wavu.

Chama cha mpira wa wavu mkoa wa Dar es Salaam DAREVA kimesisitiza mabadiliko ya tarehe pili Julai ya kuendelea kwa mashindano ya mkoa iko pale pale.

Katibu mkuu wa DAREVA Yusuf Mkarambati amesema awali walisimamisha michuano hiyo kwa muda wa wiki mbili kutokana baadhi ya timu shiriki kukabiliwa na michuano mingine ya taifa ambayo sasa imemalizika.

Mkarambati ambaye pia ni kocha wa mchezo huo amesema waliamua kusimamisha ligi hiyo kwa muda huo na kutangaza tarehe hiyo mpya ili kutoa fursa kwa vilabu shiriki vya majeshi kushiriki michuano ya mkuu wa majeshi iliyomalizika hivi karibuni.

Aidha amesema sababu nyingine ilikuwa ni kuwapa pia fursa timu ya Makongo sekondari ambao nao walikuwa wakitaraji kushiriki michuano ya UMISETA Taifa ambayo imesitishwa na Serikali ili kupisha utatuzi wa tatizo la madawati katika shule za msingi na sekondari kote nchini.

Akimalizia Mkarambati amesema pamoja na kusitishwa kwa michuano ya UMISETA kamwe hawawezi kubadili tarehe ya kuendelea michuano hiyo ama kurudisha nyuma kwakuwa tayari walishaipangwa kufuatana na ratiba za michuano hiyo ambayo inemalizika mwishoni mwa mwezi huu.