Ijumaa , 14th Nov , 2014

Dirisha Dogo la usajili kwa Vilabu shiriki vya Ligi kuu Tanzania Bara linatarajiwa kufunguliwa kesho.

Akizungumza jijini Dar es salaam,Mkurugenzi wa mashindano wa Shirikisho la Soka nchini TFF,Boniface Wambura amesema usajili huo wenye maana ya kuimarisha vilabu,vilabu vinatakiwa kusajili kutokana na idadi ya wachezaji walionao.

Wambura amesema timu zinatakiwa kuwa na wachezaji wasiozidi 30 na wasiopungua 18 hivyo kama timu itakuwa na idadi kubwa ya wachezaji haitaruhusiwa kufanya usajili huo utakaokamilika Desemba 15.