Alhamisi , 1st Dec , 2022

Uongozi wa Dodoma Jiji umsema kuwa utaanza kutumia Uwanja wa Jamhuri, Dodoma kwenye mechi za nyumbani baada ya kufunguliwa.

Uwanja huo ulikuwa umefungiwa kwa matumizi kutokana na kutokidhidi vigezo hivyo kufunguliwa kwake ni baada ya vigezo kukamilika.

Afisa Habari wa Dodoma Jiji, Moses Mpunga amesema kuwa wamepokea taarifa hizo kwa furaha na itakuwa ni mwanzo wao kuendeleza burudani nyumbani.

“Tumepokea barua ya kufunguliwa Uwanja wa Jamhuri hili ni jambo jema na zuri kwa kweli kikanuni Uwanja wa Liti ulikuwa wa nyumbani lakini ni kama tulikuwa ugenini vile.

“Disemba 12 tutaanza kuutumia uwanja huo ikiwa ni baada ya kukaguliwa mchezo wetu dhidi ya Ruvu Shoting Desemba 3 tutatumia Uwanja wa Liti.