Alhamisi , 23rd Sep , 2021

Droo ya mtoano hatua ya 16 bora kombe la Carabao imewekwa hadharani baada ya michezo ya mzunfuko watatu kukamilika usiku wa kuamkia leo, Westham United yawatoa ushamba Manchester United kwa kuwafunga 1-0 Old Trafford wakati Chelsea wakishinda penalti 4-3 dhidi ya Aston Villa.

Kombe la mashindano ya Carabao la nchini England.

Arsenal walipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya AFC Wycombe, Tottenham Hotspurs wakiwatoa Wolves kwa penalti 3-2 baada ya sare 2-2 dakika 90 wakati ambao Leicester City ilishinda 2-0 Milwall.

Baada ya matokeo hayo droo ya Carabao ilipangwa usiku wa kuamkia leo ambapo Westham United wamepangwa na Manchester City wakati Chelsea wamepangwa kucheza na Southapton Wanderers.

Droo ya hatua ya 16 bora ya kombe la Carabao inataraji kuchezwa Oktoba 25 hadi 26, 2021.