Jumatatu , 26th Aug , 2019

Droo ya hatua ya 16 bora ya michuano ya Sprite Bball Kings 2019 inayofanyika kwa msimu wa tatu mfululizo ikiandaliwa na East Africa TV na East Africa Radio kwa ushirikiano na kinywaji cha Sprite, imefanyika leo, Agosti 26 katika ofisi za EATV, Mikocheni Jijini Dar es Salaam.

Droo ya hatua ya 16 bora, Sprite Bball Kings 2019.

Jumla ya timu 16 zimeshiriki katika droo hiyo, ambapo timu 15 zilizofuzu kutoka hatua ya mtoano, zimeungana na mabingwa watetezi, Mchenga Bball Stars.

Droo nzima ya timu zilizopangwa kucheza hatua ya 16 bora ya michuano ya Sprite Bball Kings 2019 ni kama inavyoonekana hapa chini.

Michezo hiyo inatarajia kupigwa Agosti 31 na Septemba 1 katika Uwanja wa Don Bosco Oysterbay, Dar es Salaam.