Ijumaa , 2nd Dec , 2022

“Mimi niendelee kuwasisitizia tu wadau wa michezo ya kubahatisha kuwa wasipotezee hii bahati ya kushiriki katika shindano letu la Chomoka na Ndinga maana kila siku tunatoa simu janja mbili na mwisho wa wiki tunatoa pikipiki mbili na mwisho wa shindano hili kutakuwa na zawadi kubwa ya gari

Na Mwandishi Wetu,

Kampuni ya michezo ya kubahatisha Parimatch Tanzania yawaasa wateja wake kuendelea kushiriki katika kampeni yao ya ‘Chomoka Na Ndinga’ ili wajiweke karibu katika kinyanganyiro cha kuwania gari mpya mpya na ya kisasa kabisa, simu janja pamoja na bodaboda.

Hayo yamewekwa wazi na Afisa Habari wa Parimatch Tanzania na Ismael Mohamed wakati alipokuwa akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi zawadi ya pikipiki kutoka katika droo ya kwanza ya shindano la Chomoka na Ndinga.

“Mimi niendelee kuwasisitizia tu wadau wa michezo ya kubahatisha kuwa wasipotezee hii bahati ya kushiriki katika shindano letu la Chomoka na Ndinga maana kila siku tunatoa simu janja mbili na mwisho wa wiki tunatoa pikipiki mbili na mwisho wa shindano hili kutakuwa na zawadi kubwa ya gari mpya kabisa aina ya Urban cruiser kutoka Toyota”, alisema Ismael.

Aidha, Ismael alisema kuwa kampuni ya Parimatch imekuja kuwaletea neema wadau wote ambao wanapendelea michezo ya kubashiri huku akisisitizia kuwa huu ndio mwaka wa kulala masikini na kuamka tajiri kwa kubashiri na Parimatch.

Kwa upande mwingine, Kampuni ya Parimatch ndio kinara wa michezo ya kubashiri mtandaoni na imekuwa ikitoa ofa kubwa ya bonasi ya 100% mpaka TZs 1,000,000 kwa wateja wapya wanaojiunga nasi! Parimatch imekuwepo nchini Tanzania tangu mwaka 2019, ikitoa huduma nzuri ikijumuisha malipo ya haraka, odds kubwa na promosheni za kusisimua kwenye soka, Kasino na Michezo ya virtual. Mbali na soka, kampuni ya Parimatch pia hutoa mamia ya matukio kila siku kwenye tenisi, UFC, mpira wa vikapu, Kriketi, baseball na michezo mingine mingi ya Live na pre-match.