Jumamosi , 17th Oct , 2020

Mshambuliaji wa zamani wa Newcastle United Shola Ameobi anaamini elimu ni muhimu katika kupambana na ubaguzi wakati ligi kuu inazindua kampeni yake ya "Hakuna nafasi ya ubaguzi wa rangi".

Mshambuliaji wa zamani wa Newcastle United, Shola Ameobi akishangilia enzi za uchezaji wake.

Mpango huo unawahimiza mashabiki kutoa changamoto na kuripoti ubaguzi wa rangi katika mpira wa miguu, na jamii pana wakiwemo nyota kadhaa wa ligi kuu wakiwa kwenye video wakiwataka wafuasi 'Pinga, waripoti, leta mabadiliko.'

Ujumbe huu wa hivi karibuni wa "Hakuna cnafasi ya  ubaguzi wa rangi" utaonekana kwenye mechi zote za Ligi Kuu zitakazochezwa kati ya Oktoba17 na 26 mwaka huu.

Kutakuwa pia na utolewaji wa elimu bure kwenye tovuti ya ligi kuu ikiwa na ujumbe wa wachezaji kama Dominic Calvert-Lewin, Neal Maupay, Divock Origi, Hamza Choudhury na Demi Stokes.

Ameobi amesema''ni muhimu kuwepo mapambano ya jumla dhidi ya ubaguzi wa rangi na ubaguzi kwani kampeni iliyozinduliwa mnamo Machi 2019, inataka kujenga kasi iliyojengwa na wachezaji tangu mwisho wa msimu uliopita kufuatia harakati za haki ya maisha kwa mtu mweusi''.