Jumapili , 19th Jun , 2016

Mshindi mara 17 wa Grand Slam Roger Federer amepokea kichapo kwa mara ya kwanza toka kwa mchezaji kinda [chipukizi] baada ya muongo mmoja wakati akijaribu kushinda kwa mara ya 8 michuano ya Grand Slam ya Halle Open mbele ya kinda Alexander Zverev

kinda Alexander Zverev akishangilia baada ya kumchapa Federer.

Matarajio ya mcheza tenisi nguli duniani Roger Federer kutwaa taji la ubingwa wa tisa wa michuano ya wazi ya Halle yamefutwa katika hatua ya nusu fainali hapo jana na kinda wa Kijerumani Alexander Zverev, ambaye amemchapa bingwa huyo mara 17 wa michuano mikubwa ya Grand Slam kwa seti za michezo 7-6, 5-7 na 6-3.

Bingwa huyo wa Kihistoria Federer, akirejea baada ya kuwa nje kwa majeruhi alitegemea kutinga fainali kama ilivyo desturi yake wakati wakujiandaa kuelekea michuano ya Wimbledon kwa mara ya 11 lakini alijikuta akizidiwa na kinda huyo mwenye miaka 19 amabye alicheza vema mchezo huo.

Federer mwenye miaka 34 hivi karibuni alikosa michuano ya wazi ya Ufaransa kutokana na kuwa majeruhi na kuhitimisha mbio zake kushiriki mara 65 michuano mikubwa ya Grand Slam.

Raia huyo wa Uswis ambaye ni mchezaji namba tatu kwa ubora duniani hakuwai kupoteza mchezo akicheza na mchezaji chipukizi kwa takribani miaka 10 tangu wakati huo aliposhindwa na kinda wawakati huo Mwingereza Andy Murray akimchapa katika michuano ya Cincinnati mnamo mwaka 2006.

Kwa ushindi huo kinda huyo Alexander ZverevWorld ambaye ni mchezaji namba 38 sasa atakutana katika fainali na mmoja kati mshindi wa nusu fainali itakayowakutanisha Mwaustria Dominic Thiem na Mjerumani Florian Mayer.