Jumapili , 6th Oct , 2019

Fainali ya Sprite Bball Kings 2019 imeendelea leo katika mchezo wa pili na kushuhudia mabingwa watetezi Mchenga Bball Stars wakiendeleza ushindi wa pili mfululizo.

Mechi ya pili ya fainali ya Sprite Bball Kings 2019

Matokeo ya mchezo wa leo uliofanyika katika Uwanja wa Ndani wa Taifa, Mchenga Bball Stars wameibuka na ushindi wa vikapu 104 dhidi ya 89 vya Tamaduni. Baraka Sadick wa Mchenga akifunga pointi 24, rebounds 5 na assists 5.

Kwa upande wa Tamaduni, mchezaji aliyeongoza kufunga pointi nyingi ni Denis Chibula ambaye amefunga jumla ya pointi 27, rebounds 6 na assist 1.

Kwa matokeo hayo, sasa Mchenga Bball Stars inaongoza ikiwa imeshinda mechi mbili na endapo itashinda mchezo wa tatu unaofuata itakuwa imejihakikishia kushinda ubingwa wa Sprite Bball Kings kwa msimu wa tatu mfululizo.

Ratiba ya mchezo wa tatu wa fainali itaendelea Jumanne ya wiki ijayo, Oktoba 8 katika Uwanja wa Don Bosco Oysterbay.