Ijumaa , 4th Oct , 2019

Mchezo wa kwanza kati ya mitano ya fainali, Sprite Bball Kings 2019 umechezwa leo katika Uwanja wa Don Bosco Oysterbay na kushuhudiwa burudani kali  na ya kutosha kutoka kwa Mchenga Bball Stars na Tamaduni.

'Game' ya kwanza, Fainali ya Sprite Bball Kings 2019

Matokeo ya mchezo huo, Mchenga Bball Stars wameibuka na ushindi wa vikapu 122 dhidi ya 121 vya Tamaduni. Baraka Sadick wa Mchenga akiongoza kwa kufunga pointi 47, rebounds 3 na assists 3.

Pia katika mchezo huo, imeshuhudiwa burudani kali kutoka kwa mastaa kadhaa wa Bongo Fleva, akiwemo Moni, Country Boy na Amber Lulu, ambao walitoa burudani kwa mashabiki waliofurika kushuhudia mchezo wakati wa mapumziko.

Mchezo huo ni wa kwanza kati ya michezo mitano ambayo inatarajia kupigwa na endapo Mchenga atashinda michezo miwili ijayo itashinda ubingwa huo, lakini matokeo yakiwa tofauti, italazimika kupigwa michezo mitano.

Ratiba ya fainali itaendelea wikiendi hii ambapo mchezo wa pili utapigwa Jumapili, Oktoba 6 katika Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam.