Jumamosi , 7th Jun , 2014

Mabingwa wa mpira wa wavu mkoa wa Dar es salaam timu ya Jeshi Stars imeomba serikali kuboresha vyama vya mpira wa wavu ili kupata timu nyingi zaidi katika mashindano mbalimbali ya mchezo huo.

wanamichezo mbalimbali wakicheza mpira wa wavu

Mabingwa wa mpira wa wavu mkoa wa Dar es salaam timu ya Jeshi Stars imeomba serikali kuboresha vyama vya mpira wa wavu ili kupata timu nyingi zaidi katika mashindano mbalimbali ya mchezo huo tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo timu nyingi ni za majeshi.

Akizungumza na Muhtasari wa Michezo, Kocha wa timu hiyo Lameck Mashindano amesema vyama vya mchezo huo vikiboreshwa timu nyingi zaidi zitaweza kushiriki mashindano katika ngazi ya wilaya hadi taifa.

Kwa upande mwingine, maandalizi ya timu za vijana zitasaidia kuimarisha mpira wa wavu katika timu hizo kama ilivyo katika timu yake ya Jeshi Stars.