Jumatatu , 22nd Dec , 2014

Chama cha Judo nchini Tanzania JATA, kinatarajia kukutana ili kuweza kujadili mipango ya mwakani kwa ajili ya koboresha mchezo huo pamoja na maandalizi ya michuano ya Judo Kanda ya Tano.

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu Mkuu wa JATA, Innocent Malya amesema katika maandalizi ya Michuano ya Judo Kanda ya Tano itakayoshirikisha Takribani Nchi sita, nchi mbili shiriki ambazo ni Zanzibar na Burundi zimeomba michuano hiyo ipelekwe mbele kwa wiki mbili.

Malya amesema nchi hizo zimeomba kupelekwa mbele kwa michuano hiyo ili ziweze kufanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya michuano hiyo ambayo inatarajiwa kufanyika Januari 20 hadi 25 Tanzania ikiwa nchi wenyeji.

Malya amesema viongozi wote wa chama watakapokutana kwa ajili ya kupanga ratiba nzima ya michuano hiyo, ndipo watajadili juu ya maombi ya nchi hizo kuomba kupelekwa mbele kwa michuano hiyo.

Malya amesema Timu ya Tanzania imeingia kambini japo kwa mafungu ambapo ni Moshi, Korogwe na Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na michuano hiyo ambapo.

Malya amewaomba watanzania kujitokeza kwa wingi katika michuano hiyo kwa ajili ya kuweza kuishangilia timu ya Tanzania ambao ni mabingwa mara mbili mfululizo katika michuano hiyo.