Jumamosi , 2nd Aug , 2014

Kambi za mabondia hasimu wa Tanzania Thomas Mashali wa Dar es salaam na Mada Maugo wa Rorya zimeendelea kutambiana zikiwa zimebaki siku chache kabla ya magwiji hao wa masumbwi hawajashuka ulingoni siku ya Nane-Nane

mabondia Mada Maugo kushoto na Thomas Mashali kulia wakiwa na rais wa TPBO Yasin Abdallah 'ustaadhi'

Mabondia Thomas Mashali na Mada Maugo ambao watapambana katika pambano maalum la nani zaidi kati yao, mpambano utakaofanyika August 8 mwaka huu jijini Dar es salaam hii leo wametambiana kila mmoja akitamba kumtwanga mwenzake siku hiyo

Mada Maugo amesema kwa mazoezi anayofanya ni lazima ataua mtu huku Thomas Mashali akiahidi kuendelea kumpa kichapo mpinzani wake huyo katika mpambano huo maalum wakuchangia elimu katika siku ya matumaini

Pambano hilo la kimataifa la ngumi za kulipwa uzito wa kati kilo 76 litakua la raundi 6 na litasimamiwa na kampuni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO LTD

Ambapo Rais wa TPBO LTD Yasin Abdallah ‘Ostadhi’ amewataka mabondia hao kukubali matokeo ya aina yoyote yatakayotokea siku hiyo na si kuanza kulalamika wakati kila mmoja amefanya maandalizi ya nguvu na kumtambia mwenzake kuibuka na ushindi.