Kauli ya Guardiola juu ya Lionel Messi hii hapa

Jumamosi , 21st Nov , 2020

Kocha wa Manchester City, Pep Guadiola amesema angependa kuona Lionel Messi akimalizia maisha yake ya soka kwenye klabu yake ya Barcelona ya Hispania kwakuwa ana maelewano mazuri ya kihistoria na klabu hiyo.

Kocha wa Klabu ya Manchester City Pep Guardiola(Kulia) akiwa na Lionel Messi wa Barcelona (Kulia) .

“Ninachotaka ni Messi amalizie maisha yake ya soka Barcelona. Napenda iwe hivyo, Natamani itokee. Lakini msimu huu atamalizia mkataba wake na sijui nini kitatokea kwenye akili yake. Ila kwasasa ni mchezaji wa Barcelona siwezi sema zaidi”.

Suala la Guadiola kuhusiwa kumsajili Messi limeibuka upya ikiwa ni siku mbili tokea anasaini kandarasi ya miaka 2 kuendelea kuifundisha Man City hadi mwaka 2023 huku ikiripotiwa Messi hana furaha hivi sasa na miasha ndani ya klabu yake hivyo anaweza akatimka na kuungana na Guadiola.

Messi na Guadiola wamewahi kufanya kazi pamoja kwa miaka minne wakati Guardiola alipokuwa anakionoa kikosi hicho na kusaidia kwa kiasi kikubwa kukuza kiwango cha mchezaji huyo na kuifanya Barcelona kushinda mataji 14 ikiwemo mataji matatu makubwa kwa msimu 'Treble' 2008-2009.

Mafanikio hayo yalimfanya Guadiola kuwa ndiye kocha aliyefanikiwa kutwaa mataji mengi kwenye historia ya klabu hiyo hivyo kuna maelewano makubwa kati ya wawili hao na wafuatiliaji wengi wa masuala ya soka wanadhani siku moja Guardiola na Messi watakaungana tena kuipa mafaniko Man City.