Ijumaa , 10th Jun , 2016

Kuingiliana kwa ratiba ya michuano ya kimataifa ya Majeshi kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati na pia ratiba ya ujio wa kocha mpya wa timu ya Taifa ya kikapu kumepelekea kuahirishwa kwa michuano ya mpira wa kikapu taifa iliyokuwa ifanyike Julai.

Mmoja wa wachezaji wa mpira wa kikapu akionyesha staili ya mtindo wa miruko[ dank]

Shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania TBF limesogeza mbele mashindano ya Taifa ya mchezo huo yaliyokuwa yafanyike jijini Dar es Salaam mwezi ujao na sasa yatafanyika mwezi Septemba mwaka huu.

Kamishna wa ufundi wa TBF Manase Zabron amesema uamuzi huo umefanyika ili kutoa fursa kwa vilabu vingi shiriki ambavyo vinatoka taasisi ya Kijeshi nchini kupata fursa ya kushiriki kikamilifu katika michuano ya majeshi kwa nchi za Afrika mashariki na kati itakayofanyika nchini Rwanda mwezi Julai mwaka huu.

Manase ambaye pia ni mkufunzi wa ndani wa mchezo huo amesema kusogezwa mbele kwa michuano hiyo kutatoa fursa kwa kocha mpya raia wa Marekani Mark Lister ambaye pia ni mkufunzi wa kiamtaifa wa mchezo huo kuwahi kushiriki katika zoezi la uteuzi wa wachezaji watakaounda kikosi cha timu ya taifa.

Kocha huyo mwenye uzoefu na michuano ya NBA nchini Marekani anataraji kutua nchini kati ya Agasti au Septemba mwanzoni ambapo pamoja na kushiriki moja kwa moja katika zoezi la kung'amua na kuteua wachezaji watakaong'ara