Jumamosi , 23rd Aug , 2014

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. Jakaya M. Kikwete amefungua michuano ya shule za sekondari kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki FEASSA ambayo imeanza kutimua vumbi hapo jana katika viwanja mbalimbali jijini Dar es salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya M. Kikwete

Michuano ya shule za sekondari kwa nchi za Afrika mashariki na kati FEASSA inataraji kuanza rasmi kesho katika viwanja mbalimbali jijini Dar es salaam ambapo kutachezwa michezo mbalimbali ikiwemo soka, netball, mpira wa mikono, rugby, mpira wa meza na michezo mingine mingi

Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya michuano hiyo toka FEASSA Kanali Celestine Mwangasi amesema maandaalizi yote yamekamilika huku pia timu zote zikiwa zimeshawasili tayari kwa mashindano hayo makubwa kabisa kwa shule za sekondari kwa ukanda wa Afrika mashariki FEASSA.

Aidha Mwangasi amethibitisha uwepo wa mgeni rasmi katika ufunguzi wa michuano hiyo mheshimiwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Kikwete ambaye ndiye atafungua rasmi michuano hiyo hapo kesho ambayo itakusanya wanamichezo wa michezo mbalimbali zaidi ya 3000 kutoka nchi mbalimbali za ukanda wa Afrika Mashariki

Kwa upande mwingine baadhi ya timu za shule za sekondari hii leo zimefanya maandalizi ya mwisho kuelekea mashindano hayo ya FEASSA ambapo muhtsari wa michezo umezungumza na makocha wa timu za Kenya na Rwanda kujua maandalizi ya timu zao kwa ujumla kuelekea michuano hiyo.

Ambapo kocha wa timu ya mpira wa mikono ya sekondari ya wasichana ya Sega toka Kenya Maranje Omondi amesema wamejipanga kuleta maajabu katika michuano hiyo msimu huu.

Naye kocha toka Rwanda Bi Grace Nyinahumunu amesema timu za Rwanda ziko katika morali ya hali ya juu na kwa maandalizi waliyofanya wana uhakika wakuibuka na ushindi mkubwa katika mashindano hayo msimu huu.