Jumapili , 25th Aug , 2019

Hatua ya mtoano ya michuano ya Sprite Bball Kings 2019 imekamilika katika viwanja vya JMK Park hii leo.

Moja ya mchezo wa mtoano wa Sprite Bball Kings 2019

Michuano hiyo inaandaliwa na East Africa TV pamoja na East Africa Radio kwa kushirikiana na kinywaji cha Sprite, ambapo katika hatua ya mtoano uliofanyika leo, jumla ya timu 15 zimepatikana.

Timu hizo zimefuzu hatua ya 16 bora ambapo zitaungana na mabingwa wa msimu uliopita, Mchenga Bball Stars.

Listi ya timu ambazo zimefuzu hatu inayofuata hizi hapa chini.

Droo ya hatua ya 16 bora ya michuano itafanyika Jumatatu, Agosti 26 katika ofisi za East Africa TV, Mikocheni Jijini Dar es Salaam. Kupata matokeo ya jumla ya kila timu kwenye michezo ya hatua ya mtoano, bonyeza hapa MATOKEO YA JUMLA YA MTOANO