Jumatatu , 1st Dec , 2014

Mchezaji Paul Kiongera wa Klabu ya Simba ya jijini Dar es salaam anatarajiwa kuelekea nchini India kesho kwa ajili ya upasuaji wa Goti.

Akizungumza na East Africa Radio, Makamu wa Rais wa Klabu hiyo, Geofrey Nyange Kaburu amesema mchezaji huyo aliyekuwa akisumbuliwa na matatizo ya Goti anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu baada ya kufanyiwa upasuaji huo.

Kwa upande mwingine Kaburu amesema, Klabu hiyo inaendelea na zoezi la usajili hivi sasa wapo katika majaribio na mchezaji kutoka nchini Gambia, Omary Mboob ambapo wanatarajia kufanya naye kazi iwapo atafuzu majaribio hayo.