Jumanne , 14th Jun , 2016

Katika kuhakikisha inafanya vema katika michuano ya msimu ujao timu ya Everton imefanikiwa kuimarisha benchi lake la ufundi mara baada ya kuingia mkataba rasmi na aliyekuwa kocha wa Southampton Ronald Koeman.

Kocha mpya wa Everton Ronald Koeman

Kocha huyo aliyekuwa na mafanikio akiwa na kikosi cha Southampton, sasa ni rasmi ametua kuchukua ujira wa kuinoa Everton msimu ujao utakaoanza mwezi Agosti mwaka huu.

Kocha huyo raia wa Uholanzi anachukua nafasi iliyoachwa na kocha Roberto Martinez ambaye alionyeshwa mlango wa kutokea baada ya kuwa na msimu unaosuasua na vijana hao wanaotumia dimba la Goodson Park.

Taarifa zinaweka wazi kuwa kocha Koeman amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kukinoa kikosi cha timu hiyo na anataraji kuingiza kitita cha paundi million 6, akilipwa kiasi cha paundi million 2 kila msimu kwa mujibu wa mkataba wake huo.