Alhamisi , 16th Oct , 2014

Ligi Daraja la kwanza Taifa ya mchezo wa Netball inatarajia kuanza leo mkoani Tanga kwa kushirikisha timu 16 kutika mikoa mbalimbali nchini.

Akizungumza na East Africa Radio,Mwenyekiti wa Chama cha Netball nchini CHANETA, Anna Kibira amesema anaamini michuano hiyo itakuwa na ushindani mkubwa kutokana na kila timu kujiandaa vizuri kwa ajili ya kuweza kushika nafasi ya juu.

Kibira amesema michuano hiyo itakayomalizika Oktoba 24, timu sita za zitakazoshika nafasi za mwanzo kati ya timu 19 shiriki zitapanda Daraja.