Alhamisi , 13th Nov , 2014

Ligi ya Mpira wa kikapu mkoa wa Dar es salaam inatarajiwa kuendelea kesho kwa kukutanisha timu za Don Bosco na JKT huku Sarvio ikicheza na Timu ya Magereza michuano itakayofanyika Uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es salaam.

Akizungumza na East Africa Radio, Makamu wa Rais wa Chama cha Mpira wa Kikapu mkoa wa Dar es salaam BD, Richard Julles amesema hivi sasa wapo katika kipindi cha kukamilisha mzunguko wa kwanza wa michuano hiyo huku wakijiandaa kwa ajili ya mzunguko wa pili.

Julles amesema timu zitaenda mapumziko ya wiki mbili hivyo watatumia nafasi ya mapumziko hayo kucheza mechi Sita ambazo hazikuchezwa kutokana na muingiliano wa ratiba katika michuano hiyo.