Alhamisi , 18th Jun , 2015

Ligi Daraja la tatu inayosimamiwa na Chama cha Soka Mkoa wa Dar es salaam DRFA inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Julai mwaka huu jijini Dar es salaam.

Katika taarifa yake, Afisa habari wa DRFA Omary Katanga amesema, wameanza maandalizi ya ligi hiyo itakayochezwa katika viwanja vya wilaya tatu za mkoa wa Dar es salaam.

Katanga amesema, wameanza ukarabati wa viwanja vitakavyotumika kwa ajili ya michuano hiyo itakayoshirikisha timu mbalimbali.

Katanga amesema, timu shiriki zinatakiwa kujiandaa ipasavyo kwa ajili ya kuleta ushindani wa michuano hiyo ambayo hapo baadaye itazalisha wachezaji wapya wengi.