Ijumaa , 26th Dec , 2014

Ligi ya Ufukweni ya mpira wa miguu visiwani Zanzibar inatarajiwa kukamilika kesho kwa kutafuta timu Nne bora zitakazoweza kushiriki mashindano mbalimbali makubwa ya ndani na nje ya nchi.

Akizungumza na East Africa Radio, Mwenyekiti wa kamati ya Beach Soka Zanzibar, Ally Adolf amesema timu hizo zimeshacheza hatua ya makundi na wanaamini watapata timu Nne bora zitakazoweza kuitangaza nchi katika mashindano mbalimbnali.

Adolf amesema, baada ya kumaliza michuano hiyo, timu zote zitaanza maandalizi ya Mashindano ya Mapinduzi ambapo kamati inatarajia kukaa hivi karibuni kwa ajili ya kupanga ratiba kamili ya michuano hiyo pamoja na kupata idadi ya timu shiriki.

Adolf amesema, katika mashindano ya Mapinduzi wanatarajia kualika nchi mbalimbali ili kuweza kupata changamoto za kiushindani katika mchezo huo na kuwakuza wachezaji wao ili kuweza kukabiliana na changamoto hizo.