Alhamisi , 2nd Apr , 2015

Shirikisho la Ngumi Tanzania BFT limechagua wachezaji 17 wanaounda kikosi cha Timu ya Taifa ya Ngumi kwa ajili ya kushiriki mashindano mbalimbali ikiwemo Mashindano ya All African Game yatakayofanyika Septemba mwaka huu cnhini Brazili.

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu Mkuu wa BFT Makore Mashaga amesema,wachezaji hao wamepatikana katika mashindano ya mbalimbali ambapo timu hiyo inatakiwa kuanza mazoezi Aprili 15 mwaka huu Uwanja wa ndani wa Taifa huku taratibu za kuandaa kambi ya muda mrefu ya timu hiyo zikiendelea.

Mashaga amesema Mabondia waliochaguliwa wametengwa kwa makundi kutokana na uzito ambapo katika Uzito wa Kilo 49 Light Fly wapo mabondia Mohamed Mzeru, Maulid Athumani na Ibrahim Abdalah huku Kilo 52 Fly Weight ikiwa na Juma Ramadhani na Said Hofu.

Mashaga amesema kwa Upande wa Kilo 56 ambayo ni Bantam Weight wapo Mabondia Ahamad Furahisha na Bon Mlinga huku Kilo 60 ambayo ni Light Weigt ikiwa na Elias Mkomwa, Bosco Bakari na Fabian Gaudence huku kilo 64 akiwa Kassim Mbwitike, Kilo 69 ikiwa na Said Gulushad na Seleman Bamtulah.

Mashaga amesema, katika Uzito wa kilo 75 ambao ni Middle Weight kutakuwa na Bondia Ivan Mussa na Kilo 81 ambayo ni Light Heavy ikiwana Hamidu Halfan huku Kilo 91 ambayo ni Heavy Weight akiwa Bondia Alex Sitta na Nuru Ibrahim..